Leo nilipata muda wa kupita madukani kuchukua baadhi ya vitu nilivyopungukiwa kwenye kazi hii ya ubunifu mavazi na vitu vinginevyo.Katika pitapita yangu nikakutana na vitambaa hivi nashangaa mate yakaanza kunitoka.Like seriously vilikuwa vinanitoa mate kuvishona.Nikavishikashika mate yakawa yanazidi.Hee!nikataka kuvikimbia maana sikwenda haswa kwa lengo la kuvinunua lakini akili ikaniambia hata usiponunua leo utanunua siku moja na utapenda kuvishona.Nikaona isiwe tabu ngoja nichezee vitambaa tofauti tofauti maana kwangu vimekuwa kama toy na nina enjoy sana.
Kitenge #19
Hiki kitenge ni cha zambarau sio blue.Isamehe camera yangu tumepiga picha usiku ikachanganya rangi zake yenyewe au ni mimi sijui kuiset usiku tusamehe mimi na camera bure.
Nilifikiria collection yangu yote ya vitambaa nikagundua sina zambarau hivyo nikakibeba baada ya kukipenda.
Chiffon #1
Hii ni chiffon.Nilivyoiona tu nikapata picha fulani kichwani nikapenda nikachukua na nyenzake kama mbili zaidi.Ya baby yellow na peach.
Chiffon #2
Chiffon #3
Satin #1
Satin #2
Mh,Stoo yangu ya vitambaa ndio inayonipa bichwa la kununua more fabrics maana ina nafasi kwelikweli.Otherwise najua ningekuwa mpole.
Napenda sana vitambaa,napenda kubuni,napenda kushona mwenyewe,napenda kufanya vitu vingi vinavyohusiana na ubunifu.
Ni nini nitashona kutoka vitambaa hivi?
Stay tuned.
Until then,maintain the chicky,classy look.....bye.
No comments:
Post a Comment