HE is The GREAT MIGHTY GOD.
Jamani,mafundi wakiwapa nguo zenu pamoja na vitambaa vilivyobaki,MSIVITUPE!Hata kama unakiona ni kidogo kuna kitu cha maana na chenye mvuto unaweza ukapata kwa kutumia udogo huohuo wa kitambaa.
Binafsi nikimshonea mtu nguo huwa namrudishia kitambaa kilichobaki(kama kipo) na 'scrapper' zake ambazo naona zitamsaidia na huwa namshauri asitupe.
Kuna vitu vingi unaweza kutengeneza kutokana na 'scrapper' za vitambaa.Unaweza kupata hereni,bow-tie,vifungo,vibanio,bangili,mikanda,zulia dogo,mapambo,n.k..n.k Na sio lazima uwe na mashine ya kushona.Hata kwa mkono vinatengenezeka kirahisi tu.
Leo nitakufundisha namna ya kutengeneza bow-tie kutumia moja ya scrapper nilizochukua haraka haraka.Nina fuko hilo la scrapper nikikuonyesha utacheka ukauke.Ila huwa linanisevu sana.Nimeona nichukue sample tu.
Baadhi ya sample za scrapper zangu
Kipande kidogo cha kitambaa nitakachotengenezea bow-tie
Kata kitambaa chako katika umbo la mstatili
Kilinganishe vizuri.Hakikisha mapana kwa mapana yamelingana,na marefu kwa marefu yamelingana.
Njia rahisi ya kufanya hivyo ni kukikunja mara mbili kama inavyoonekana hapo.Halafu kata kiusawa pande zinazohusika.
Geuza kitambaa ndani nje.Kuna pande tatu zitakuwa wazi.Shona mbili,acha hiyo moja wazi hivyohivyo.
Pande iliyowazi itakusaidia kugeuza kitambaa chako.
Tengeneza vizuri kona na sehemu zote ilikopita mashine ili shepu ionekane vizuri.
Nyoosha kitambaa chako,kitokee na shepu nzuri zaidi.Mojawapo ya siri ya ufundi wa nguo ipo kwenye kunyoosha mapindo kila unaposhona.
Unaona ile sehemu ya wazi iliyobaki?Kunjia kitambaa ndani,kilingane vizuri,
Kisha shona kupafunga,ukizunguka kitambaa kizima.
Kitambaa kiko tayari na kina shepu ya mstatili.Kata kitambaa kingine katika saizi ndogo kama hapo juu...
Na chenyewe,shona ndani nje
Geuza ndani nje.Unaweza kutumia hata pini ya nguo...ile inayofanana na pini za nepi za watoto.
Ikunje katikati ilingane,halafu shona ukiunganisha juu na chini ili iwe duara dogo
Ingiza katikati ya kitambaa kile cha mwanzo na hii ndio bow-tie yetu.
Unaweza kutumia hii kama kibanio pia.
Kwa kifupi mabaki ya vitambaa yana msaada na kama nilivyosema,sio lazima uwe na mashine ya kushonea nguo ili kupata vitu vidogodogo kama hivi,vingi vinafanyika kwa sindano ya mkono kabisa tena vinatoka nadhifu.
Mpaka wakati ujao,stay classy,Love each other.Bye.
No comments:
Post a Comment