Nimekuwa bize mnisamehe tu nimechelewa mpaka ku-post nimepata nafasi mchana huu.Nina nguo za watu za kutengeneza,ni nyingi kiasi ila ninazimudu.
Nimeona si vyema sana nguo nazotengeneza na vitu vinginevyo ikiwemo pochi,viatu,sandals kuendelea kutembea mtaani bila kuwa na label zangu.Baadhi ya wateja wanaulizwa umeshonewa na nani wanasema 'sijui dada gani yule ana blog yake fulani hivi ya fashion yule dada yule wewe humjui?' Hee? Hapo sasa inakuwa 'makubwa!'
Nipo kwenye mchakato wa kuchagua rangi bado.Ila label inafanania hivi.
Ipo simple.Ina logo ya TrendyDecentMe! By Margareth Tarimo. I am proud in a humble way.Thank you LORD.
Naziweka sehemu ambazo mtu anaweza kuonyesha kirahisi bila kujali ni aina gani ya nguo imevaliwa.
Bize bize bize michuchumio leo hapana maana nahitaji ku-move haraka na kwa wakati.
Vitu vizuri sana vinakuja.Kuwa mvumilivu kidogo..Kimya kingi kina mshindo mkuu.
Thank you LORD.
Mpaka wakati ujao,stay classy....Bye.
No comments:
Post a Comment