Sunday, July 6, 2014

Nogesha Sandals zako Na Margareth Tarimo





HE is The ALMIGHTY  LORD GOD worthy to be Honored.

Tupo kwenye weekend ndefu kidogo,siku tatu,maana kesho ni sabasaba na nimefurahi kupata muda mzuri na Mungu,familia,marafiki pamoja na kupumzika.Oh nilimisije kulala jamani na leo nilivyotoka kanisani tu nimeuchapa vizuri  mnoo kabla ya kujumuika na familia na marafiki na usiku nitalala sana tu.I deserve it.Kama unakimbizana kila siku unahitaji muda wa kupumzika pia.Huu ndio umri wa kuwa farasi  maana baada ya kama miaka 30+ huko itakuwa wakati wa kulinda boma kama mbwa huku nakula kivulini,ila nimegoma kuzeeka.Natia ngumu mapema,huu mwili na sura tuelewane kabisa mapema,'No uzee'.Umri uongezeke,sawa lakini 'No Uzee'.Siri iko kwenye kula 'sensibly',mazoezi hata kidogo tu kwa wiki inasaidia,kunywa maji mengi,kupumzika masaa yanayotakiwa na kumcha Mungu.Hii ya mwisho unaweza ukaguna lakini ndio uhalisia.Nitaizungumzia vizuri siku nyingine.



Kwa kweli leo sikuwa na mudi sana ya kukaa mbele ya kamera,japo nilikuwa nimekutayarishia vitu vizuri mnoo.Kuna siku kweli unaamka 'u just don't feel the camera,the flash etc' na picha huwa zinatoka hohehahe ukilazimisha.Since nina vitu vingi vya kukupa,nikaona nikuonyeshe jinsi sandals zako ambazo wewe unaziona ni za kawaida sana,zikafanywa kuwa sandals zenye mvuto mno za kutokea.Nikanogesha na ile wallet niliyowahi kuipost huko nyuma mambo yakanoga.

Noga hivi na Margareth Tarimo...



















                      MY DESIGN,MY FASHION,MY PASSION-Margareth Tarimo

Umependa?
Whatsup +255 712 484508

Mpaka wakati ujao,jijali,jipende,jithamini....Bye

No comments:

Post a Comment