Tuesday, July 29, 2014

Simple Blouse By Margareth Tarimo




How marvellous is your NAME O LORD!

So,jana usiku nilikuwa nimechoka kiasi,ila nina hamu ya kushona.Nina nguo za wateja ila sithubutu kuzigusa wakati nimechoka.Baada ya kucheza na wanangu sana,nikaanza kuwabembeleza walale,yule mkubwa alikubali akalala fofofo..hawa wadogo wakaniwekaje sasa..wamekuja kulala saa saba usiku tena kwa lazima.Wakati tunabembelezana na nikaona hakuna dalili ya wao kulala,mie huyo nikaanza kupekua natafuta vitambaa nishone chochote tuu..Nikakipata hiki hapa...


Huyu mwanangu anapenda sana kujifunza.Utasikia 'mamaaa, shona.'Nikiwa nakata anaangalia akichoka anachukua madaftari yake anaandika hapo hapo habanduki utashangaa baadae anauliza ulikata mita ngapi?umefanya finishing?(lol!)..na huwa najibu maswali yake.

Japo nilikuwa nimechoka,nilikuwa na hamu ya kushona.Nikaona hako kakitambaa nishone blauzi simple tu




                                    Kipande cha mbele tayari





                                  Kipande cha nyuma


                                 Imeanza kutokea lakini haina mikono


                                 Ramani ya Mikono


Hapa sawa kabisa,na finishing nimeshafanya.Iko poa.Nilipomaliza kushona niliridhika sana hamu ya kushona ikapungua nikapata usingizi sasa.

Coming up next....Kodac Moments....


 Nikajivalia zangu polka-dot shoes na hair clip...










MY DESIGN,MY FASHION,MY PASSION-Margareth Tarimo

Tutaonana wakati ujao...Nawatakia wote Eid Mubarak njema.Stay classy.Bye.

Saturday, July 26, 2014

JumpSuit With Ankara Flavor By Margareth Tarimo




HE is The Faithful GOD.

Yani kupiga picha hizi ilikuwa ni full burudani.Maana mpiga picha alikuwa hana mbavu kila nikipozi,halafu kulikuwa na kaupepo basi yani anacheka karibu akauke jinsi hili surupwete linavyotepweta.Mimi mwenyewe nilikuwa hoi kwa kucheka.It was so much fun!

Niliwaahidi kuwa nitashona 'kanya humohumo' au jumpsuit hivi karibuni.Ahadi ni deni.Kama kawaida nimetupia na kitenge.Kitenge kwangu ni kama chumvi kwenye chakula.lol!..Haya sasa,hilo hapo muhangaike nalo wenyewe.













 Mbavu zangu!..uwii...naiogopa fashion sasa.







 Kiruu!nauliza tena..umeshawahi kuona mtoto wa kama mwaka mmoja na nusu aliyeachia mizigo yake kwenye pampers jinsi suruali yake inavyomshuka??...






Fashion.It's all about generating good ideas every moment.Some may be funny though.Ila nimejitahidi kuliremba  lipo poa sana halafu lipo soo comfortable.Yani sana.Litanisitiri nikiwa napeleka wanangu shule na kwenda shopping za hapa na pale.Kama unadhani langu ni kituko,angalia hili fungakazi sasa...


                             Asante sana.

Yeah,wakati mwingine fashion ni vichekesho.Tuvae tuchekeshe wengine,wanenepe,waongeze maisha.

Mie kama umelipenda nakushonea tena kali kweli kweli!Tutafutane whatsup +255 712 484508.
Mpaka wakati ujao,stay classy....Bye.

Thursday, July 24, 2014

How To Make A Bow Tie - Namna Ya Kutengeneza Bow Tie




HE is The GREAT MIGHTY GOD.

Jamani,mafundi wakiwapa nguo zenu pamoja na vitambaa vilivyobaki,MSIVITUPE!Hata kama unakiona ni kidogo kuna kitu cha maana na chenye mvuto unaweza ukapata kwa kutumia udogo huohuo wa kitambaa.

Binafsi nikimshonea mtu nguo huwa namrudishia kitambaa kilichobaki(kama kipo) na 'scrapper' zake ambazo naona zitamsaidia na huwa namshauri asitupe.

Kuna vitu vingi unaweza kutengeneza kutokana na 'scrapper' za vitambaa.Unaweza kupata hereni,bow-tie,vifungo,vibanio,bangili,mikanda,zulia dogo,mapambo,n.k..n.k Na sio lazima uwe na mashine ya kushona.Hata kwa mkono vinatengenezeka kirahisi tu.

Leo nitakufundisha namna ya kutengeneza bow-tie kutumia moja ya scrapper nilizochukua haraka haraka.Nina fuko hilo la scrapper nikikuonyesha utacheka ukauke.Ila huwa linanisevu sana.Nimeona nichukue sample tu.

Baadhi ya sample za scrapper zangu

Kipande kidogo cha kitambaa nitakachotengenezea bow-tie

Kata kitambaa chako katika umbo la mstatili

Kilinganishe vizuri.Hakikisha mapana kwa mapana yamelingana,na marefu kwa marefu yamelingana.

Njia rahisi ya kufanya hivyo ni kukikunja mara mbili kama inavyoonekana hapo.Halafu kata kiusawa pande zinazohusika.

Geuza kitambaa ndani nje.Kuna pande tatu zitakuwa wazi.Shona mbili,acha hiyo moja wazi hivyohivyo.

Pande iliyowazi itakusaidia kugeuza kitambaa chako.

Tengeneza vizuri kona na sehemu zote ilikopita mashine ili shepu ionekane vizuri.

Nyoosha kitambaa chako,kitokee na shepu nzuri zaidi.Mojawapo ya siri ya ufundi wa nguo ipo kwenye kunyoosha mapindo kila unaposhona.

Unaona ile sehemu ya wazi iliyobaki?Kunjia kitambaa ndani,kilingane vizuri,

Kisha shona kupafunga,ukizunguka kitambaa kizima.


Kitambaa kiko tayari na kina shepu ya mstatili.Kata kitambaa kingine katika saizi ndogo kama hapo juu...


Na chenyewe,shona ndani nje

Geuza ndani nje.Unaweza kutumia hata pini ya nguo...ile inayofanana na pini za nepi za watoto.


Ikunje katikati ilingane,halafu shona ukiunganisha juu na chini ili iwe duara dogo



Ingiza katikati ya kitambaa kile cha mwanzo na hii ndio bow-tie yetu.

Unaweza kutumia hii kama kibanio pia.

Kwa kifupi mabaki ya vitambaa yana msaada na kama nilivyosema,sio lazima uwe na mashine ya kushonea nguo ili kupata vitu vidogodogo kama hivi,vingi vinafanyika kwa sindano ya mkono kabisa tena vinatoka nadhifu.

Mpaka wakati ujao,stay classy,Love each other.Bye.

Sunday, July 20, 2014

Tupia Kitenge Ndani Ya Kitambaa Cha Suti Hivii...




HE is The Mighty GOD.

Wazo hili lilinijia ghafla wakati nashona vitambaa vya suti siku za nyuma,kwamba,naweza kutupia ladha ya kitenge kidogo kwenye kitambaa cha suti na kikapendeza.Sasa kwa kuwa mimi napenda makoti,nikaona nitengeneze koti nitupie halafu tuone inakuajekuaje.Nikajiuliza nalitupia kivipi maana sikutaka koti lijae sana kitenge.Nikapata wazo ya koti ambalo nataka nitupie kitenge mahali fulani fulani,nikaprint picha yangu,nikai-modify navyotaka mimi.

Nilitaka sehemu ya chini tu ya koti kutoka kwenye hiyo picha hapo.Nikaanza kuchora vipimo kama kawaida..


Nilitaka liwe na nakshi za vifungo vya kitenge mikononi,mbele na nyuma.Hivyo nikatengeneza vifungo vyangu vitano kama vinavyoonekana pichani

 Nikaona si haba nishone na sketi ya nguva kabisa aka 'mermaid skirt' na nikanogesha na kwenye pochi pia,tayari mie huyoo nimemaliza.
































My natural hair....free-style.Nimekuwa nikipata maswali kuhusu utunzaji wa nywele asilia mara kwa mara.Nitakuja kuzungumzia na hili pia.Kwa kifupi,utunzaji wa nywele asilia ni rahisi zaidi na salama kabisa ukilinganisha na matunzo ya nywele bandia au zenye dawa.Hii mada nitakuja kuiongelea muda si mrefu.

Endelea kutembelea humu kama kawaida.Umependa mishono?whatsup yangu hiyo hapo kulia.
Mpaka wakati ujao,stay classy.Bye.