Mungu ni Mwema Sana.Leo ilikuwa harusi ya yule dada Happy niliyekuwa kwenye ile kitchen party yake juzi.Wamependeza,harusi imefana sana!Ukumbi ulijaa mno na vyakula,vinywaji vilikuwa vya kusaza!
Rangi za harusi zilikuwa tatu;Zambarau,Nyekundu na Gold.Unaweza vaa zote kama ukiweza kupatia kuchanganya,au ukavaa mbili kati ya hizo.Lakini pia ilikuwa ruksa kujimwaga kwa rangi yoyote utakayopenda wewe.
Mimi nilijivalia zangu Zambarau,na Gold,nikatupia accessories nyekundu.
Kama kawaida macho ya camera yalijaribu kuangalia watu walivyotokelezea na pia kutafuta my favorite print yaani #Kitenge ,#Chitenge,#Tenge,#Ankara nikapata pozi chaache za haraka maana kulikuwa na shamrashamra mno hata mimi kupiga picha watu sikuweza.
Mama kijana kama mwanae huyu chini....
They look like sisters but one of them is actually a daughter..
Bado natafuta #Vitenge jamani...
No #Ankara today?
If u couldn't figure out earlier,this is 'The Mom'
Finally nikakutana na #Kitenge cha rangi za shughuli,na kimetendewa haki
Asante sana
#Ankara ya ukweli.....Wadesaji mishono tupo?
Kila la kheri dada Happy na shemeji yetu,tunawatikia ndoa yenye upendo,amani na maelewano.
Uwii..inabidi nilale sasa hivi ni saa saba na robo usiku na ninatakiwa niamke saa kumi na mbili kamili ili niwahi ibada ya pili saa tatu kamili.
Until then,stay classy...
No comments:
Post a Comment