Sunday, June 22, 2014

Dress Suit,Ankara Coat By Margareth Tarimo



                      #ANKARA   #VITENGE  #CHITENGE  #SUITDRESS  #KENTE

How Marvellous is your Name O LORD!

Baada ya kuongeza vitambaa vya suti kwenye stoo yetu,nikapata hamu ya kushona kitu ambacho nitaweza kutupia na koti la kitenge na kikanoga.So,katika kupekua stoo nikapenda kitambaa cha suti #53 na kitenge #42.Kitenge nikashona koti la kutupia juu ya suti ambayo iko katika mtindo wa kigauni,nikanogesha na mkanda wa gold,na kapochi ka gold,(inategemea wapi unaenda)na hivi ndivyo vilivyotokelezea.

Tokelezea namna hii na Margareth Tarimo!

 Wakati naanza kuchora vipimo kwenye kitambaa kabla ya kuanza kukikata.Mafundi mpo?!...lol!


  Muonekano wa mwisho.Imeshakuwa kagauni ka suti.Mabegani kuna nakshi ya virinda viwili nilisahau kukuonyesha.viko poa sana,vinapendezesha kiaina.


 Nikatupia na koti la kitenge.Unaweza kwenda hivi kazini au hata kwenye mitoko yako mingine na ukaonekana nadhifu kabisa.


 Napenda huo urembo wa mbele wa gauni la suti.Na finishing ya suti?safi kabisa.Tiki.Vema.





 Zoom....


 Hapa kwenye mtoko unaenda,kanisani,na kokote mbali na kazini.Kipochi cha mkononi kimeshakunogesha.





                      MY DESIGN,MY FASHION,MY PASSION-Margareth Tarimo

Glory to God for the wonderful works of my hands.
Umependa muonekano huu?

Whatsup +255 712 484508

Until then,maintain the classy look....Bye.

No comments:

Post a Comment