Sunday, June 8, 2014

Kitenge Ndani Ya Kikoti

                   #ANKARA #VITENGE #KENTE #CHITENGE #AFRICANPRINTS

 How Excellent Is Your Name O Lord!

I wish ungekiona hiki kikoti live maana ni kizuri zaidi ya picha inavyoonyesha.Wakati nashona nilikuwa nimechoka ajabu maana ilikuwa usiku,lakini kilipoisha nikakijaribu yani nimekipenda mpaka nusura nilale nimekivaa.Kikanipa nguvu mpya ya kukata kitambaa kingine.

Picha zenyewe za leo nimepiga haraka haraka maana nilikuwa na ishu nyingiii nikiangalia ratiba niliyonayo mbele kesho sitapata muda wa kupiga picha basi ikabidi niibinyie ratiba ya picha kwenye ratiba ya leo basi dah..picha zenyewe ndo hivyo hivyo..

Nimechezea kitenge #38 kutoka kwenye stoo yetu ya vitambaa.Kuchungulia stoo yetu bonyeza 'MY FABRICS' pembeni ya Home page.

Pendeza namna hii,Tokelezea na vitambaa vya nyumbani.










            Hapa huenda nilikumbuka ratiba 'taiti' iliyopo mbele yangu,nikakonda akili ghafla







Kikoti hiki unaweza kuvaa na jeans ukanoga mnoo..Ilibaki robo inch nikurushie muonekano wake lakini nimeona nitakupa flavor hiyo wakati mwingine maana kwanza nitashona vingi tuuu...Kaa mkao huo huo endelea kuchungulia humu.

Mpaka wakati ujao,keep looking trendy but classy!

Kutoa oda Whatsup @ (+255) 712 484508

Bye.

No comments:

Post a Comment