Friday, August 8, 2014

Namna Ya Kuondoa Stika Kwenye Vitambaa-How To Remove Cloth Stickers


HE is An Awesome GOD.

Nimekaa chini leo nikakumbuka jinsi huko nyuma kabisa kabla sijaanza kushona, kuna siku nilihangaika sana na stika kwenye kitambaa ikatoka vibaya vibaya ikararuka ikaacha weupe usiopendeza.Nikaona nikupe hili somo dogo kama hukulifahamu,ili uondokane na adha kama niliyoipata mimi huko nyuma.

Unaondoaje Stika zinazokuja na vitambaa especially,vitenge?

1.Weka kitenge chako mezani.Chukua pasi yako,washa moto mdogo kabisa kwenye pasi.



2.Ikishapata joto weka juu ya stika iliyopo kwenye kitambaa chako kwa kama sekunde 5-7


3.Anza kuvuta stika yako taratibu utaona inatoka kiulaini bila nguvu yoyote



4.Na hivi ndivyo kitambaa chako kitabaki.Safi kabisa



5.Kumbuka kuweka pasi yako kwenye moto mdogo kabisa kukuepushia kuharibu kitambaa


Nakutakia siku njema.

Mpaka wakati ujao,nunua vitambaa quality na origino....Stay classy...Bye.

No comments:

Post a Comment