LORD,I love you.
Guess who is featured in here today?A male kid...and yes,MY son.Got three of em'.Full security..u dare touch me..lol!
I thank The LORD ALMIGHTY and I am so proud,in a humble way.
Juzi mchana nilikuwa napanga nguo nikagundua natakiwa kuongeza sare za huyu dogo.Nikaona ngoja niikamilishe hii kazi leoleo maana sidhani kama ningepata muda tena.
Nikaenda kununua vitambaa vya sare yao ya shule,nikatoa vifaa vichache nje,kubadili mazingira,kupata fresh air...wow! kushonea nje kuna raha yake ndio maana mafundi nguo wengi huku bongo utawakuta nje.Fresh air,stories,kuna raha yake.
Kipande cha mbele cha kaptula
Kipande cha nyuma cha kaptula
Kaptula imekamilika,nikahamia ndani,maana ilikuwa tayari giza limeingia
Shati likimaliziwa
Mie hoi na mapozi ya watoto,mara midomo,mara mikono...
Hako ka mkono kake ka kulia sijui ndio kamewekwa clockwise mpaka kamegota.Haya,safari ya shule inaanza.Uzuri shuleni sio mbali kwa mguu kunaendeka ila ndio magari na pikipiki barabarani
Kashaona kitu,anataka kuokota.Kasahau yuko na mimi.Hilo begi huwa nakuta spare parts za karibu vitu vyote ulimwenguni kuanzia screw,bolt,misumari, mpaka mifuniko ya chupa na anajua kuvificha.Kama ukibahatika kukuta chochote humo ujue umekuta sample tu.Mzigo kamili umeshahifadhiwa siku nyingi.Usiku ndio siri zinapofichuka.Nikishawaacha chumbani walale huwa nazima taa.Hapo ndipo anapoibua makorokoro yoote anamwaga kitandani wenzie wanam join kuyachezea.Muda si muda wanajisahau, wanagombana ,wananyang'anyana.Napoenda nione kulikoni makelele yote hayo,ndipo napopata suprise ya moyo.Makorokoro yote kitandani,tena mengine ya hatari,live bila chenga.Nina kazi.
Yeah,uniform for pre-scholars by TrendyDecentMe!.Soon natangaza nafasi ya fundi mzuri,nitaweka requirements zote hapa...mzigo unaanza kuwa mzito kidogo sasa...na nina mambo mengi mno ninahitaji angalau mmoja kwanza,tuone ana-'handle' vipi kazi.
Mpaka wakati ujao...let your children shine in their school uniforms by TrendyDecentMe!.
Do not forget to stay classy,Bye.
No comments:
Post a Comment