Thursday, October 15, 2015

Join Me In The Weight Loss Program-Ungana Nami Kupunguza Uzito




Habarini Za masiku watu wangu wa nguvu.Nimewamisi sana.

Nilikuwa kimya kidogo,maana majukumu yalinizidi kimo.Si unajua maisha ni kujituma na kuhakikisha kila idara ime balance vyema yani Mungu,Kazi,Familia,Marafiki,Afya Yako,n.k

Sasa katika mahangaiko hayo,nikawa nakula kinachopatikana tu,sikuzingatia sana ni aina gani ya chakula nachokula mfululizo.Nikirudi nyumbani ni usiku nalala.Asubuhi nikiamka ni kujitayarisha,ndani ya gari,mbio ofisini.No mazoezi,No diet watching.Matokeo yake,NIMENENEPAAAA!!Jamani nimenenepa.Nguo nyingine nilizovaa mwaka uliopita december tena kwa kuzishona mwenyewe hazinitoshi!Nimeongezeka kilo 13 ndani ya miezi 11.HAIKUBALIKIIIII.SITAKIIIII.



Kwa hiyo wiki iliyopita  nikaanza kuangalia vyakula kwa umakini zaidi.Sijinyimi kula,nahakikisha nashiba,ila nakula mlo 'Salama' yani healthy foods na kunywa maji mengi pamoja na mazoezi ambayo sio mazito sana kama kutembea haraka na kukimbia.Pamoja na hayo,unatakiwa kuwa unahesabu 'Calorie' zako kwa siku ambazo unahitaji kuzi maintain ili uweze kupungua.Kuna Applications nzuri sana tu kwenye internet ikiwemo 'MyFitnessPal' ambayo mimi ninaitumia.



Kwa haraka haraka nikiamka nakunywa kikombe kimoja cha maji vuguvugu yenye mdalasini,tangawizi kidogo,(sio ya unga) na yaliyokamuliwa nusu kipande cha limao.Ni kwamba niliweka mdalasini kijiko kidogo 1 na tangawizi,(sio ya unga)wakati maji yametoka kuchemka.Yakifikia vuguvugu ndio naweka limao.Mimi naweza kuyanywa hivyo lakini kama unaona hayapiti kooni unaweza kuweka kijiko kidogo 1 cha asali mbichi.Baada ya lisaa nakula chakula chenye 'whole grain' kama weetabix cereals pamoja na maziwa yaliyoondolewa mafuta yani 'Skim Milk' au Fat free milk.Chagua cereals zenye low fat na low sugar.Mwili ukiendelea kupiga kelele za njaa nakula karoti moja mbichi.Then nakunywa maji mengi sana.



Naona nisiendelee kuandika maana page itajaa sana.Bado mchana,jioni ngoja nikupe summary ya mlo wangu kwa siku kama inavyoonekana kwenye diary yangu ya 'MyFitnessPal'.
Hizo weetabix utazipata supermarket nyingi tu wanazo au unaweza kuangalia cereals/oats nyinginezo ambazo ni low calorie na low sugar.Hilo chupa hapo juu ni 3.5ltrs na ni lazima nilimalize kwa siku na tena naongeza kama glass mbili.Uzuri ni kwamba napenda maji.








Nitaziondoa kilo 15 kwa awamu kwa wastani wa kilo 4 mpaka 5 kwa kila mwezi.Kupungua haraka sana na ghafla sio vyema kitaalam.Kuna madhara.Kwa ambao mpo interested,tunaweza kufanya pamoja.Kuibia madikodiko kumo mara moja moja sana (sio uibie sufuria zima) lakini hakikisha unatoa calorie zilizoongezeka kwa mazoezi.Kama hutafanya mazoezi basi uwe strict sana na diet.


Ngoja niishie hapa kwa leo,nakutakia siku njema na karibu sana kwenye program ya kupunguza uzito.

Sunday, August 17, 2014

Other Projects Came Up...



The LORD is awesome...

So,I am happy and sad at the same time.Happy that I got more projects to work on,sad that I 've a very very limited time here....sijawarushia mambo yetu yale kwa muda kidogo.Hii ni kwa sababu miradi mingine imeingilia kati ikiwemo nguo za wateja,nakimbizana nazo.

Soon,nitawaletea tena vitu vizuri,ila kwa sasa nadhani itakuwa mara moja kwa wiki nawarushia.Nikiweza zaidi ya hapo it's well and good.

Stay tuned...endelea kutembelea humu.

Do not forget stay classy as well.
Your designer,
  Margareth

Tuesday, August 12, 2014

Amazing Creative Ideas With Nail Polish-DIYs-Tumia Rangi Yako Ya Kucha Hivi



Glory To GOD for we are still alive!

Jana usiku nilikuwa natafuta kitu,nikachukua mfuko mmojawapo nikakuta rangi zangu za kucha nyingiiiii nimeziweka.Nikasema nita-share na nyie ideas nzuri muone jinsi ambavyo unaweza kutumia rangi zako za kucha kupendezesha vitu vingine ukiachia kucha.


Wengi wetu (wanawake) tunapaka rangi ya kucha kupendezesha muonekano wa vidole.Lakini tujiulize hivi kweli huwa tunatumia mpaka zinaisha?Unakuta mtu ana rangi tofauti tofauti nyingi(mie mmojawapo) ila ni kweli tunatumia mpaka zinaisha au zinaishia kuganda wakati mwingine?

Zifuatazo chini ni 'ideas' unazoweza kufanya mwenyewe ukapendezesha vitu vyako vingine ukiachia kucha.Have fun!!

1.Remba vidani,hereni,mikufu.





Vitu vingine unatengeneza hata dakika 10 haziishi unakuwa na kitu chenye mvuto na 'unique'


2.Pakaa kwenye 'head-phones' za simu yako...wow!!(yes wow!..i know u said it)



3.Pakaa kwenye cover la simu yako.Hakikisha unapaka 'quality' original color else ikitoka magambamagamba usijenikamata koo..lol!



Unaweza kumwagia mng'ao ikawa hivi..



Au ukamwagia shanga na viurembo vingine ikawa hivi....



5.Ile pochi yako inayokuboa kisa iko soo plain unaikumbuka?Ifanyie hivi...






6.Miwani yako imeanza imepoza?Iweke hivi...




7.Tengeneza hereni,vidani kutoka kwenye kachuma kale ka vibanio vya nywele....



8.Kikombe chako usikisahau...



Na vinginevyo vingi vingi....Save your cash .

Have a blessed day,stay classy,accessorize your stuffs with nail polish.Bye.

Friday, August 8, 2014

Namna Ya Kuondoa Stika Kwenye Vitambaa-How To Remove Cloth Stickers


HE is An Awesome GOD.

Nimekaa chini leo nikakumbuka jinsi huko nyuma kabisa kabla sijaanza kushona, kuna siku nilihangaika sana na stika kwenye kitambaa ikatoka vibaya vibaya ikararuka ikaacha weupe usiopendeza.Nikaona nikupe hili somo dogo kama hukulifahamu,ili uondokane na adha kama niliyoipata mimi huko nyuma.

Unaondoaje Stika zinazokuja na vitambaa especially,vitenge?

1.Weka kitenge chako mezani.Chukua pasi yako,washa moto mdogo kabisa kwenye pasi.



2.Ikishapata joto weka juu ya stika iliyopo kwenye kitambaa chako kwa kama sekunde 5-7


3.Anza kuvuta stika yako taratibu utaona inatoka kiulaini bila nguvu yoyote



4.Na hivi ndivyo kitambaa chako kitabaki.Safi kabisa



5.Kumbuka kuweka pasi yako kwenye moto mdogo kabisa kukuepushia kuharibu kitambaa


Nakutakia siku njema.

Mpaka wakati ujao,nunua vitambaa quality na origino....Stay classy...Bye.

Monday, August 4, 2014

Uniform za Mwanao Na TrendyDecentMe! By Margareth Tarimo




LORD,I love you.

Guess who is featured in here today?A male kid...and yes,MY son.Got three of em'.Full security..u dare touch me..lol!

I thank The LORD ALMIGHTY and I am so proud,in a humble way.

Juzi mchana nilikuwa napanga nguo nikagundua natakiwa kuongeza sare za huyu dogo.Nikaona ngoja niikamilishe hii kazi leoleo maana sidhani kama ningepata muda tena.

Nikaenda kununua  vitambaa vya sare yao ya shule,nikatoa vifaa vichache nje,kubadili mazingira,kupata fresh air...wow! kushonea nje kuna raha yake ndio maana mafundi nguo wengi huku bongo utawakuta nje.Fresh air,stories,kuna raha yake.








                                Kipande cha mbele cha kaptula


                               Kipande cha nyuma cha kaptula


                              Kaptula imekamilika,nikahamia ndani,maana ilikuwa tayari giza limeingia


                                                     Shati likimaliziwa


                 Mie hoi na mapozi ya watoto,mara midomo,mara mikono...    


 Hako ka mkono kake ka kulia sijui ndio kamewekwa clockwise mpaka kamegota.Haya,safari ya shule inaanza.Uzuri shuleni sio mbali kwa mguu kunaendeka ila ndio magari na pikipiki barabarani


Kashaona kitu,anataka kuokota.Kasahau yuko na mimi.Hilo begi huwa nakuta spare parts za karibu vitu vyote ulimwenguni kuanzia screw,bolt,misumari, mpaka mifuniko ya chupa na anajua kuvificha.Kama ukibahatika kukuta chochote humo ujue umekuta sample tu.Mzigo kamili umeshahifadhiwa siku nyingi.Usiku ndio siri zinapofichuka.Nikishawaacha chumbani walale huwa nazima taa.Hapo ndipo anapoibua makorokoro yoote anamwaga kitandani wenzie wanam join kuyachezea.Muda si muda wanajisahau, wanagombana ,wananyang'anyana.Napoenda nione kulikoni makelele yote hayo,ndipo napopata suprise ya moyo.Makorokoro yote kitandani,tena mengine ya hatari,live bila chenga.Nina kazi.


               
Yeah,uniform for pre-scholars by TrendyDecentMe!.Soon natangaza nafasi ya fundi mzuri,nitaweka requirements zote hapa...mzigo unaanza kuwa mzito kidogo sasa...na nina mambo mengi mno ninahitaji angalau mmoja kwanza,tuone ana-'handle' vipi kazi.

Mpaka wakati ujao...let your children shine in their school uniforms by TrendyDecentMe!.
Do not forget to stay classy,Bye.

Friday, August 1, 2014

Get This Look With Margareth Tarimo



 Thank you LORD.

Kuna wakati mtu unajisikia kuvaa 'casual'...No formal look.
Unaweza ukapigilia kitenge chako namna yoyote ambayo wewe mwenyewe utakuwa 'comfortable' na umejisitiri.Unaweza ukavaa kasuruali ka kitenge na ukapendeza.

Leo sikuwa na mudi ya masketi,magauni au whatever.Mizunguko na vishughuli nilivyokuwa navyo pamoja na hali ya hewa,vilinilizimu kuvaa hivi na yes,nimepata compliments za kutosha na wamependa muonekano huu.Baada ya hapo mie huyoo na shughuli zangu.

Pata muonekano huu na Margareth Tarimo.







                      Mummy yao nani huyu?
                      Hint: ADD you decode the names.

Big Up to my photographer Shahidi Mwandembo,owner wa OurVoice Blog.Pata habari motomoto na zenye uhakika kutoka http://www.ourvoicetz.blogspot.com/

Until then,maintain the casual look,Bye.

Tuesday, July 29, 2014

Simple Blouse By Margareth Tarimo




How marvellous is your NAME O LORD!

So,jana usiku nilikuwa nimechoka kiasi,ila nina hamu ya kushona.Nina nguo za wateja ila sithubutu kuzigusa wakati nimechoka.Baada ya kucheza na wanangu sana,nikaanza kuwabembeleza walale,yule mkubwa alikubali akalala fofofo..hawa wadogo wakaniwekaje sasa..wamekuja kulala saa saba usiku tena kwa lazima.Wakati tunabembelezana na nikaona hakuna dalili ya wao kulala,mie huyo nikaanza kupekua natafuta vitambaa nishone chochote tuu..Nikakipata hiki hapa...


Huyu mwanangu anapenda sana kujifunza.Utasikia 'mamaaa, shona.'Nikiwa nakata anaangalia akichoka anachukua madaftari yake anaandika hapo hapo habanduki utashangaa baadae anauliza ulikata mita ngapi?umefanya finishing?(lol!)..na huwa najibu maswali yake.

Japo nilikuwa nimechoka,nilikuwa na hamu ya kushona.Nikaona hako kakitambaa nishone blauzi simple tu




                                    Kipande cha mbele tayari





                                  Kipande cha nyuma


                                 Imeanza kutokea lakini haina mikono


                                 Ramani ya Mikono


Hapa sawa kabisa,na finishing nimeshafanya.Iko poa.Nilipomaliza kushona niliridhika sana hamu ya kushona ikapungua nikapata usingizi sasa.

Coming up next....Kodac Moments....


 Nikajivalia zangu polka-dot shoes na hair clip...










MY DESIGN,MY FASHION,MY PASSION-Margareth Tarimo

Tutaonana wakati ujao...Nawatakia wote Eid Mubarak njema.Stay classy.Bye.