Nimekuwa bize bize bize!Hii kazi inahitaji muda wangu sana na niko tayari kuipa kabisaa maana kwanza naipenda kutoka moyoni.Ninashona nguo zenu wateja wangu,ninashona nguo zangu za 'photoshooting',nashona mchana,nashona usiku.Kushona kushona kushona!..Mimi huyu huyu naenda shopping kutafuta materials.Naanza kufikiri kuajiri lakini ngoja...kuna quality fulani ya mishono nataka ambayo kwanza nishone mwenyewe labda nikizidiwa kupita kiasi ndio nitatangaza nafasi ya fundi.
Jana nikiwa katika mizunguko yangu madukani nikakutana na kitambaa kimoja ambacho siyo kitenge lakini kikanivutia na ghafla akili yangu ikanionyesha mshono wa kutumia kabla hata sijakinunua.Nikawa impressed kukichukua.
I wonder how this will turn out...
Sehemu yangu ya kazi
Najitahidi kuweka vitu mpangilio maana nisipoangalia kila mahali patajaa nyuzi,vitambaa,pini,masarasara ya mabaki ya vitambaa na vyote unavyovikutaga kwa mafundi nguo.
Nashona usiku.Mwanangu huyu kanizoeaje sasa?Nikiwa nyumbani ni kama kivuli changu.Wenzake aaah hawana shida.Labda kwa sababu ni pacha hivyo wanapeana kampani wenyewe.Kila Niendapo huyu yupo nyuma yangu.Hata nikishona usiku na yeye habanduki pembeni.Utasikia mama naomba nikae na wewe...niwekee katuni.Uzuri ni kwamba ilikuwa ni usiku wa ijumaa kuamkia jumamosi.Hatakiwi shuleni.Otherwise ingebidi nimkazie macho makubwa ili akalale kwa lazima.
Kaeni mkao wa kupendeza....Tailor in shift 15 hrs a day,6 days a week.Ndio 15/6..ndio yangu hiyo.Inaweza kubadilika pia..hehehe..
Until then,maintain the classy,chicky look....bye.
No comments:
Post a Comment