Sunday, June 29, 2014

ColorBlock SuitDress Na Margareth Tarimo




HE is The faithful GOD.

Weekendi imekwenda vizuri namshukuru sana Mungu.Nimepata muda mzuri mno na Mungu na familia yangu.

Vitambaa vya suti navyo ni wow!..Napenda jinsi vilivyo vitiifu kwenye kushona haswa kama ukipata fundi wa ukweli na mbunifu.Nilipoingia stoo yetu bloguni nilivutiwa na  vitambaa vya suti namba 44,45,55 na 57 na nilipoibuka mambo yakawa ifuatavyo...

Noga kihivi na Margareth Tarimo.










 Uwii yani photographer wangu ni anavichekesho mpaka kupiga picha inakuwa full burudani.Huwa najikaza sana kucheka lakini nashindwa,afterall,kucheka kunaongeza maisha na afya njema.Wanasema 'Laughter is a medicine'


                      MY DESIGN,MY FASHION,MY PASSION- Margareth Tarimo

Yes,vitu vikali namna hii vinapatikana kwangu.
Kutengenezewa hivi,whatsup +255 712 484508.

Nashona nini wakati ujao?...stay tuned.
Until then,maintain the chicky,classy and decent look,Bye.

Wednesday, June 25, 2014

Dress Suit in Black & Indigo-Blue By Margareth Tarimo


                      #DRESS SUIT

HE is The HOLY LORD,worthy to be honored.

Namshukuru sana Mungu maana pamoja na ubize wote nilionao,ninapata nguvu ya kukuletea mambo kama haya na kukupendezesha.Kweli nguvu nilizonazo ni 'beyond normal' kwa hiyo narudi palepale Mungu nakushukuru sana.

So,nilizama katika stoo yetu ya vitambaa nikajisikia kuondoka na vitambaa vya suti viwili #44 inaitwa 'Indigo-Blue' na #45 cha Black.Kuona stoo yetu ina nini click MY FABRICS pembeni ya Home hapo juu.

Nikavikalia kwa masaa kadhaa na hivi ndivyo vilivyotokelezea.
Pendeza namna hii na Margareth Tarimo and Yes,Classy.


                     The left side of the dress suit


                     The right side of the dress suit


                      The Back.

                 
                                The bottom





                     MY DESIGN,MY FASHION,MY PASSION-Margareth Tarimo

Yani ndio kulikua kumekucha asubuhi ikabidi nifanye photoshooting wakati nimelala saa nane kasoro usiku wa manane na baada ya hapo ni kazini.Lakini namshukuru Mungu nimeamka nina nguvu kabisa,so fresh.

Vitu vizuri vinakuja,kaa mkao wa kupendeza.

Umependa muonekano huu na ungependa kupendeza hivi?
Whatsup +255 712 484508

Until then,maintain the chicky,classy look,LOVE GOD.....Bye.

Sunday, June 22, 2014

Dress Suit,Ankara Coat By Margareth Tarimo



                      #ANKARA   #VITENGE  #CHITENGE  #SUITDRESS  #KENTE

How Marvellous is your Name O LORD!

Baada ya kuongeza vitambaa vya suti kwenye stoo yetu,nikapata hamu ya kushona kitu ambacho nitaweza kutupia na koti la kitenge na kikanoga.So,katika kupekua stoo nikapenda kitambaa cha suti #53 na kitenge #42.Kitenge nikashona koti la kutupia juu ya suti ambayo iko katika mtindo wa kigauni,nikanogesha na mkanda wa gold,na kapochi ka gold,(inategemea wapi unaenda)na hivi ndivyo vilivyotokelezea.

Tokelezea namna hii na Margareth Tarimo!

 Wakati naanza kuchora vipimo kwenye kitambaa kabla ya kuanza kukikata.Mafundi mpo?!...lol!


  Muonekano wa mwisho.Imeshakuwa kagauni ka suti.Mabegani kuna nakshi ya virinda viwili nilisahau kukuonyesha.viko poa sana,vinapendezesha kiaina.


 Nikatupia na koti la kitenge.Unaweza kwenda hivi kazini au hata kwenye mitoko yako mingine na ukaonekana nadhifu kabisa.


 Napenda huo urembo wa mbele wa gauni la suti.Na finishing ya suti?safi kabisa.Tiki.Vema.





 Zoom....


 Hapa kwenye mtoko unaenda,kanisani,na kokote mbali na kazini.Kipochi cha mkononi kimeshakunogesha.





                      MY DESIGN,MY FASHION,MY PASSION-Margareth Tarimo

Glory to God for the wonderful works of my hands.
Umependa muonekano huu?

Whatsup +255 712 484508

Until then,maintain the classy look....Bye.

Friday, June 20, 2014

Stoo Ng'aring'ari!Vitambaa Zaidi Vimeingia



Vitambaa vichache vimeingia leohii vikiwa ni mchanganyiko wa vitenge,suti,lace na vile vya kuvutika(lycra).Uwii,sijawahi shona nguo ya kuvutika nina hamu ya kuichezea.Vitambaa vya suti ni wow!..Napenda sana kuvichezea maana vinakubali sana mashono.Kati ya vitambaa vitiifu kwangu mimi ni vya suti.

Stoo ng'aringari!

























Sipati picha nguo nitakazotoa kutoka kwenye vitambaa hivi!..mate yananichuruzika,nina hamu ya kuvikata,kuvishona.
Kaa mkao wa kuona mambo mazuri.
Unti then,maintain the classy look.....Bye.


Wednesday, June 18, 2014

Mshono 'Simple' Na Kanga

                      #KANGA                         #KHANGA                        staili #1

HE is a Mighty GOD!

Leo nikaingia katika stoo nikaondoka na kitambaa #30 ambacho ni kanga nikatamani nishone kigauni 'simple' ambacho unaweza kukifunga kwa staili zaidi ya kumi.

Kikatokelezea kama hivi...unaweza kuvaa na sandals au hata ukaamua kutokelezea na kiukweli kweliii na viatu ...

Onja ladha tofauti za mavazi na Margareth  Tarimo.


                     #Kanga  #Khanga                                               staili #2


                       side view                                  #Kanga  #Khanga

                      staili #3                                           #Kanga  #Khanga


                      staili #4                                     #Kanga  #Khanga


                      #Kanga  #Khanga

Hii kanga unaweza kufunga staili tofauti zaidi ya 10 na pia unaweza kuivaa kama sketi peke yake.
Nimewaonjesha tu, nitatafuta muda nitakuonyesha ufungaji tofauti wa hii kanga.

Kaa mkao huohuo vitu vizuri mnoo vinakuja...yani mimi mwenyewe nipo excited!Nashona huku mate yananidondoka maana vimeanza kutokelezea kweli kweli!

Umependa mshono?Whatsup +255 712 484508

Until then, maintain the chicky,classy look...Bye

Sunday, June 15, 2014

Pendeza Na Kitenge Chako Hivi Na Margareth Tarimo


             
The LORD Reigns!

So,katika post iliyopita ya kikoti niliwaahidi nitawarushia muonekano wa kikoti cha kitenge na jeans.Nikazama ndani ya stoo yetu ya vitambaa(Kuona stoo click MY FABRICS pembeni ya Home page) kuchagua rangi itakayonivutia nikatoka na kitenge #7 na hivi ndivyo kilivyotokelezea.

Pendeza namna hii na Margareth Tarimo.























                         MY DESIGN,MY FASHION,MY PASSION-Margareth Tarimo

Sina la ziada,picha zimeongea.Umevutiwa na matumizi ya kitenge?

Kuoda, whatsup +255 712 484508

Until then,maintain the classy look,LOVE GOD and people.....Bye.


Friday, June 13, 2014

Kitenge Ndani Ya Wallet

                                #ANKARA #VITENGE #AFRICAN PRINTS #KENTE

Nina wallet yangu moja ninaipenda sana halafu imedumu ina miaka kama minne sasa kama si mitano.Haijachanika,ila hivi karibuni ilianza kuwa na rangi haieleweki kama ni nyekundu (kama nilivyoinunua) au ya kahawia.Nilipoichunguza nikagundua ni nzima kila kona,haijachanika isipokuwa rangi tu ndo imeanza kusumbua.

Mimi tena?Kama kawa.Balbu ikawaka kichwani na hivi ndivyo ilivyotokelezea...

                                Mbele


                               Finishing safi kabisa hakuna manyuzinyuzi


                               Nyuma


#teamrecycle mpo? #hakunakutupakitu  #designerkapatikana

Pata design mpya na Margareth Tarimo

Until then,maintain the classy,chicky look....LOVE GOD and people.Bye.